Wednesday, 26 December 2012

COSTA SIBOKA ATAMBULISHA WIMBO WAKE MPYA MOSHI

 
MSANII Costa Siboka 'Mfalme wa muziki wa asili'  katikati akicheza na watoto alipofanya ziara yake wakati wa sherehe za Krismas mjini Moshi.
Ambapo alifanya utambulisho wa wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina la 'Watoto Wangu' ndani ya ukumbi wa kisasa unaokimbiza Mo-Town unaoitwa Zumba Land .
Costa alifanikiwa kuwapagawisha wakazi wa Moshi kwa kiasi kikubwa ambao kwa kiasi kikubwa waliongozana na watoto wao hata kumfanya ashangiliwe kila dakika.

Costa Siboka ameahidi kuusambaza uhondo huo katika mikoa ya Iringa, Mbeya na Songea kuanzia mwisho wa mwezi Machi mwakani (2013).

Aidha, Mfalme huyo ameahidi kuimba nyimbo zingine kupitia makabila ya Kihehe, Kinyakyusa, Kingoni na nyingine.

Msanii huyu nyota aliyewahi kutwaa taji la Mr Guiness ukanda wa Afrika Mashariki, amekuwa akipata udhamini wa nguvu toka kampuni kubwa ya bia nchini (TBL), Konyagi na Precision Air.


Sunday, 23 December 2012

CHAMUITA WAZINDUA WEBSITE YAO



Rais wa (CHAMUITA) Addo November, katikati  Mweka Hazina Upendo Kilahiro  na Naibu Mwenezi John  Shabani.

Na Khadija Kalili

MAPEMA wiki hii Rais wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania (CHAMUITA)  Ado November ameitaka serikali kutokukimbilia mchakato wa kufanya usajili kwa kazi za wasanii kwa kutumia stika moja bila ya kuweka mipango madhubuti ya kuwabana wezi wa kazi hizo.

Akizungumza jana Dar es salaam November anasema kwamba Serikali isikimbilie katika stika pekee bali watupie kwanza macho ya kazi za wasanii zinazoibiwa sehemu mbalimbali kama kwenye mabasi, ambako huoneshwa filamu na CD za miziki ya Injili huku msanii akiachwa bila ya kupata faida yeyote.

“Sio hao ntu bali wezi wengine ni pamoja na waumini wakuu wa  dini ya Kikristo kwani nao utawaona wakitoka katika nyumba za kuabudu Kanisani wanalipia fedha kidogo huku wakidurufiwa CD huku wakichagua ,majina ya wasanii  wanaotaka nyimbo na picha zao ,utasikia wakitoa orodha ya majina ya nyimbo na albamu wanazozitaka, katika hili hata mungu hatoweza kupokea sadaka zao wanazozitoa makanisani kwani wanafanya dhuluma kwa watu wanaojinyima na kurekodi lakini wao badala ya kununua albamu nzima wanaishia kuchoma CD” anasema  November.

Anaongeza kwa kusema ,”Sisi  kama CHAMUITA tumejipanga  kuwekeza  katika elimu zaidi ili wasanii wa muziki wa Injili waweze kufahamu haki zao  kwanza kabla ya kuingia katika mpango huo ambao ni mzuri kimaendeleo.

Wakati huohuo November anasema   CHAMUITA wamepiga hatua  kubwa kwani hadi sasa tayari wameshszindua ‘website’  ya chama itakayofahamika kama www.gospal Tanzania.com ambapo wasanii ambao ni wanachama wataweza kujitangaza  kwa kuuza picha, nyimbo na zao kwa kupitia mtandao huo


Wakati huohuo mjumbe wa CHAMUITA , Bahati Bukuku amezungumza kwa niaba ya waimbaji wengine wa muziki wa Injili kwamba serikali sikurupuke katika suala la uanzishwaji wa kutumia stika moja kwani itawabebesha mzigo wasanii na kazi zitaendelea kuibiwa zaidi.


“Wizi wa kazi za sanaa ni janga la Taifa hivyo kila Mtanzania anapaswa alipigie kelele, hiki ni kilio cha umma sisi wasanii hatukubaliani kwamba kila msanii atatumia stika moja , hapo wizi utaendelea kwanini wasitumie mfano wa kadi za benki huku kila mmoja akawa na namba au neno lake la siri ili  kila msanii ajue anakwatwa kodi kwa namna gani  na kwa kutokana na kopi ngapi  kulingana na kipato chake lakini ikiwa stika moja wapo wasanii watakaopandia kwa kupitia jina la mwingine”anasema Bukuku.

MALENGO NA MADHUMUNI
November anasema CHAMUITA Itaendeshwa kama chombo kisicho na malengo ya kupata faida na kitakuwa na malengo na madhumuni yafuatayo anayoyataja, Kulinda utamaduni wa Tanzania na heshima ya muziki wa Injili, Kuhamasisha maendeleo ya muziki wa Ijili na nyaja zake nyingine,Kutoa ushauri katika mambo yote yahusuyo muziki wa Injili.Kuwakilisha na kulinda maslahi ya wanachama kitaifa na kimataifa, Kuwa chombo cha kuwezesha mawasiliano kati ya watu na vikundi katika kupeana taarifa kuhusu muziki wa Injili, Kuwa na rejista ya wanamuziki wa Injili na kazi zao.  Ili kusaidia kulinda na kutangaza haki za wanachama, Kutafuta mapato kwa njia ya ada, michango, harambee, maonyesho, kukopa, ufadhili au zawadi katika kuendeleza malengo na madhumuni ya Chama, Kuwezesha mawasiliano ya kitaifa na kimataifa, Kuwawezesha wanamuziki wa Injili kwa njia ya kuwaongezea elimu, Kuinua hadhi ya muziki wa Injili nchini,Kutambuliwa rasmi na Serikali yetu na wadau wengine Tayari tumesajiliwa na BASATA na kupewa usajili rasmi na  Kuwekeza katika miradi, na kujipatia kipato kwa nia ya kuwakomboa jamii ya wanamuziki wa injili.

 Changamoto kwa wasanii

Wasanii mbalimbali ambao walihudhuria mkutano uliratibiwa na Mamlaka ya Mapato nchini (TRA), walilazimika kutofikia muafaka katika mkutano huo na baadhi ya viongozi waliofika kuzungumzia mpango wa uwekwaji wa stika ifikapo mwakani.

Chama chetu kinaundwa na Mwanamuziki mmoja mmoja yaani solo artist, vikundi, umoja wa Makundi yote ya Muziki  wainjili hapaTanzania, kwa kuhusisha radio, watangazaji, wapigaji na wadau wa muziki wa injili.

Safu ya uongozi (CHAMUITA ) Addo November ,Makamu Mchungaji Joseph Malumbu , Katibu  David Robert ,  Katibu Mwenezi  Stella Joel, Naibu Mwenezi John  Shabani, Mweka Hazina Upendo Kilahiro.

Wajumbe wa Kamti Kuu  wako zaidi  ya 60 huku baadhi ni  wakiongozwa na  Mbunge Matha Mlata, Mzee  Makassy, Cosmus Chidumule, Bahatgi Bukuku, Ency Mwalukasa, Christine Shusho, Levina Steven, Mzee Mutash, Jojo Josee , Jackson Bent, Fred Rwesasira.

Mikakati ya Chama
November anasema kuwa tayari wameshazungumza na wanachama wao ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ambayo wamejiwekea ambayo ni kuunganisha wanamuziki wote wa injili na wadau wao na kuwapa nguvu katika majukumu yao ya kila siku, pamoja na kutetea haki za msingi za wanamuziki.

Kuwakumbusha wanamuziki juu ya umuhimu wa CHAMA na kuishi maisha ya kumpendeza Mungu, Kutetea haki za wanamuziki na kutoa wito kwa jamiii na serikali kwa ujumla wa kutambua wizi wa kazi za sanaa kama janga la kitaifa kwani wanamuziki wanakosa mapato na serikali inakosa kodi ambayo inaweza kuzidi hata mapato ya maliasili na utalii au madini, mfano kazi moja tu ya mwanamuziki mmoja akauza nakala milioni 4 kati ya watanzania milioni 40 waliopo mwanamuziki huyo anaweza kupata bilioni 4 kwa kanda ya shilingi 1000 tu.

November  anasema tunaungana na kauli hii ya Shirikisho la Muziki Tanzania kuwa umefika wakati sasa wanamuziki tuseme basi katika kuibiwa kazi zetu  za sanaa , tunawataka  viongozi  wan chi wakae  pamoja  nasi tuwape mikakati yetu  wasikae mbali  na sisi kwani tuna uwezo  wa kukuza uchumi.
Kutoa mafunzo kwa wanamuziki kuhusiana na muziki na haki miliki, pamoja na kuwekeza katika maisha  ya baadaye  tayari kuna wadau kutoka LAPF  tayari wametoa mada na kuandikisha wanachama, hii ni fursa kwao kujipatia mikopo ya nyumba na kuwekeza katika akiba yao ya baadae.
Kutoa mapendekezo juu ya mabadiliko ya sheria yetu ya haki miliki ambayo kiukweli haina meno na imepitwa na wakati. Leo tunatoa dukuduku chetu juu ya Sheria inayolinda kazi za wanamuziki na wasanii wengine (The Copy Rights and Neighbouring Act no 7 of 1999) mfano suala la faini isiyozidi milioni tano, kwani sheria haisemi kazi hizo feki zinapelekwa wapi na faini hii imekuwa ndogo mno na pia inatoa mwanya kwa watafsiri sheria ambao mara nyingi tumejionea wakitoa hukumu ya mwizi kulipa faini ya laki mbili au elfu sabini na kurudishiwa kazi yake ya wizi maana sheria ipo kimya.
Tunatoa pongezi wa Rais Kikwete kwa kukubali mchango wa Chama mcha muziki wa injili na kukubali kuwa chama pekee kilichoshiriki kuimba katika miaka 50 ya uhuru pale uwanja wa taifa.
Hata hivyo tunatoa rai kwa viongozi wa serikali kushirikisha makundi mbali mbali ya sanaa katika mchakato mzima wa kutetea haki za wanasanaa wote kwani hiii itawapa fursa kufanya mambo yatakayokidhi haja za wanamuziki na sanaa kwa ujumla.
Tunawashukuru wanamuziki wa injili na wdau mbali mbali kwa jinsi walivyojitoa katika kumzika mzee wetu, Remmy Ongala, waandishi waliopata ajali wa radio za injili ambapo chama kilijitoa kuwaona na kuwafariji,  msiba wa Fanuel Sedekia na kusaidia waathirika wa Gongo la Mboto kazi hii ilifanyika kwa ufanisi mkubwa na mzee wetu Remmy alizikwa kwa heshima kubwa, tunawaomba tuzidi kushikamana.
“Tunashukuru  sasa tumezindua uzinduzi website ya kwanza kutoka kwa wanamuziki wa Tanzania, ambayo ni www.tanzaniagospel.com iliyotengenezwa na Kampuni ya Spice Olyympus.
 pamoja na haya bado tunajipanga kuwatafutia wanamuziki wa injili mafunzo zaidi ya kuwafanya kujitegemea na kusaidia maendeleo ya nchi” anasema November

Mwisho November anamalizia kwa kutoa pongezi za dhati na shukrtani kwa LAPF kwa kudhamini mkutano wao  na kuwaomba wanachama kuwaunga mkono katika jitihada  zao za kuwa komboa  watanzania.

MUIMBAJI WA MUZIKI WA IN JILI ALIYEDHALILISHWA KIJINSIA


DONNIE Mc Clurkin ni Mwanamuziki Mashuhuri wa nyimbo za Injili na Mchungaji wa Kanisa la Perfecting Faith church lililopo katika jimbo la Detroit nchini Marekani.
Donnie alizaliwa na familia ya Donald na Mama Frances Mcclurkin Januari 25, mwaka  1959 na kukulia katika mji wa Louisville.
Akiwa na umri wa miaka nane, mdogo wake wa kiume mwenye umri wa miaka miwili aligongwa na gari na kufa papo hapo huku Donnie akishuhudia.
Wakati Donne akiwa na majonzi mazito usiku huo huo ambao walimzika mdogo wake, mjomba wake alimbaka Donne.
Baada ya kifo hicho familia yake iliingia kwenye mgogoro kubwa ambao ulitokana na utumiaji wa dawa za kulevya.
Muimbaji huyo alipofikisha miaka 13, binamu yake mtoto wa mjomba wake alimbaka tena Donnie pamoja na dada zake wawili kitendo amabacho kilimuumiza sana na kumuachia kovu la aina yake.
Anasema kuwa muda wote alijiona mkosaji, mtu aliyekandamizwa na hakuwa na ujasiri mbele za watu na mwenye wingi wa aibu.
Kwa kipindi hicho chote anaeleza kuwa alipata faraja toka kwa shangazi yake ambaye alikuwa muimbaji wa nyimbo za Injili.
Shangazi yake huyo alimfanya Donnie ajiingize kanisani na kuanza kupiga piano na kuimba kwaya kama sehemu ya kufuta machungu na kuondokana na msongo wa mawazo aliokuwa nao.
Mama yake mzazi naye alikuwa muimbaji kanisani hivyo kanisani kukawa ndio nyumbani kwake na kambi yake pindi nyumbani kukitokea matatizo.

Julai 14, 1969 akiwa na miaka takribani kumi ikiwa ni jumapili akiwa kanisani huko Amityville Gospel Tabernacle mtumishi wa Mungu aliyekuwa akihubiri aliwaambia watu kuwa Kristo alikufa kwa sababu anakupenda wazo  hilo ndilo lilikuwa kwa Mcclurkin ndipo akaamua kuyakabidhi maisha yake kwa Yesu.
Kwenye kitabu alichoandika kuhusu maisha yake anasema “ Kanisa limekuwa ndio ulimwengu wangu mahali ambapo najisikia amani na najisikia kama ndio Mahali Pangu halisi”anaeleza.
Mwaka 1971 wakati ana miaka 11, alikuwa akimpenda sana mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za injili kipindi hicho aliyeitwa Anre Crouch.
Anaeleza kuwa siku aliposikia kuwa Crouch anakuja katika jimbo lao alimuomba mama yake ruhusa waende kwenye tamasha na kumuahidi jumatatu yake ataamka mapema na kwenda shule kama kawaida.
Anaendelea kusema kuwa mama yake alikubali na wakaenda Tamashani na Donnie akaaa mbele kabisa sambamba na mamaye.

Baada ya Crouch kuingia ukumbini saa tano usiku kabla hajaanza kuimba alimuona Donnie na kumfata, Donnie anasema, “Crouch akaniuliza kitu gani unafanya hapa, nikamjibu nakusubiri wewe, akaniuliza kama nimelipenda tamasha nikamjibu ndio, akanambia wakati yuko mdogo hakuweza kuimba wala kucheza mpaka baba yake alipomuombea, Nikamjibu baba yangu hajaokoka hivyo hawezi kuniombea. Mwishoni akaniuliza kama nitapenda aniombee nami nkamkubalia akaweka mkono wake kichwani kwangu akasema “Mungu mpe kile ambacho umenipa mimi” kisha akaelekea stejini, huuo ulikuwa ndio mwanzo wa hiki nlichonacho leo”anasema Donnie.

Akiwa kanisani hapo alianzisha kundi llilokuwa linajulikana kama The Mcclurkin Singers na baadaye alianzisha kundi lililokuwa likijulikana kama The New York Restoration Choir.
Mwaka 1983 wakati akiendelea kutumika na kwaya alikutana na Pastor Marvin Winans.
Mchungaji Winans alivutiwa sana na namna Donnie alivyokuwa akiimba kwenye semina ya injili.
Baadaye Winans alimwalika Mcclurkin katika mji wa Detroit alikokua akiishi ili kumsaidia kuanzisha huduma kanisa liitwalo Perfecting Faith Church.
Miaka sita baadaye Donnie aliamua kuhamia Detroit na kuanza kufanya kazi na Pastor Winans.
Katika kipindi hicho anasema kuwa ndipo Mcclurkin alipata wasaa wa kuzunguka sehemu mbalimbali na kufanya huduma akiwa chini ya pastor Winans.
Donnie anasema familia ya Winans imekuwa karibu sana na yeye Kuanzia Bebe, Cece, na Pastor Marvin na wakati mwingine anafikiri yeye ni Donnie Mcclurkin Winans.
Donnie Mcclurkin na Cece Winans wakiwa wameshikilia tuzo za Trumpert awards walizopewa mwaka 2007
Akiwa na Pastor Winans, alisaini mkataba na kurekodi albamu yake iliyoitwa LP, Albamu hiyo iliyokuwa na nyimbo kama Stand iliyongoza kwa umaarufu na kuzinduliwa na Oprah Winfrey.
Nyimbo hiyo ilitunukiwa tuzo ya Grammy kwa mwaka huo wa 1996 kwa upande wa nyimbo za Injili. Album zake tatu za solo zilikamata nafasi za juu sana kwenye chati za Bilboard.
Akiwa na furaha ya ajabu Mcclurkin kupitia makongamano mbalimbali huwasimulia watu ukweli wa maisha yake huku akipinga kwa nguvu mahusiano ya jinsia moja.
Mcclurkin anaamini kwamba suala la Homosexuality ni suala la kiroho haliwezi tibika kisaikolojia na linahitaji msaada wa Mungu pekee. Baada ya watu wengi kuwa wanamuomba aelezee historia ya maisha yake, Mcclurkin aliamua kurudi nyumbani kwao Amityville New York na kumuomba Mama yake ruhusa ili aandike kitabu kuhusu maisha yake.
Frances Mcclurkin (mamaye), alimruhusu Donnie aandike kitabu kinachoyaelezea maisha yake kinaga ubaga, ndipo Mcclurkin akatumia miezi 18 kuandika kitabu hicho ambacho alikiita Eternal Vitcting, External Victor. Alisema aliamua kuandika kitabu sio kwa kusudi la kuweka wazi uovu uliokuwa ukifanyika ndani ya Familia yao bali kwa sababu yeye ni Mwalimu, na mwalimu ni vizuri ajitoe yeye kama ujumbe ili watu wengine wajue kuwa hawako peke yao kwenye mambo wanayopitia.

Mwaka 2008 Mcclurkin alichaguliwa kuwa miongoni mwa wanamuziki ambao watakuwa kwenye timu ya Barak Obama katika harakati za uchaguzi wa nchini Marekani.
Mcclurkin alikubali na kujumuika na Barak Obama, lakini kutokana na msimamo wake wa kupinga mahusiano ya jinsia moja, Mashoga wengi walipinga kuwepo kwake kwenye timu ya Obama. Hivyo ili kupata kura za mashoga ilibidi Mcclurkin atolewe kwenye orodha hiyo ingawa alifanikiwa kuimba kwenye moja ya kampeni za Rais Obama
Makala hii imeandikwa kwa msaada wa mtandao na Happiness Mnale, 0712 00 35 39,barua pepe mnaleh@yahoo.com
mwisho

NYIMBO ZA INJILI ZILIZOTIKISA 2012


Na Betty Kangonga

UNAPOZUNGUMZIA albamu ya nyimbo za muziki wa injili zilizofanya vema kwa mwaka 2012 ni pamoja na iliyoibwa na mwimbaji wa nyimbo za injili ambaye anakuja juu anayefahamika kuwa ni Enock Jonas.

Moja ya nyimbo inayofanya vizuri na ambayo imekuwa ikipigwa katika sherehe mbalimbali na hata hafla ni ile inayokwenda kwa jina la  wema wa Mungu ‘Zunguka Zunguka’.

Jonas ambaye katika albamu hiyo amefanikiwa kutunga nyimbo zingine nane ambazo ni ufanikiwe, ukimtegemea Mungu, Haleluya
nakuabudu Bwana, ndugu zangu, ni vyema na ile inayosema leo ni furaha.

Mwimbaji mwingine ambaye albam yake inaendelea kufanya vema ni malkia wa nyimbo za injili nchini Rose Mhando ambaye aliitambulisha album yake ya nne inayokwenda kwa jina la Utamu wa Yesu.

Albam hiyo ambayo inafanya vema katika vituo mbalimbali vya redio na televisheni za ndani na nje ya nchi.

Mhando katika nyimbo yake ya Utamu wa Yesu na raha ya ajabu anasema “Nimeonja utamu wa Yesu, Ukitaka gari nzuri, majumba mazuri onja utamu wa Yesu”.

Kama usemi mmoja unavyosema kuwa aliyenacho anaongezewa ndivyo ilivyokuwa kwa mwaka huu kwa upande wa malkia huyo kwani aliweza kuingia mkataba mnono na kampuni ya Sonymeingia mkataba mnono na kampuni mahiri katika masuala ya muziki na burudani hapa ulimwenguni,Sony Music.

Rose Muhando ambaye anakuwa msanii wa kwanza wa muziki wa injili nchini Tanzania kuingia mkataba wa kampuni ya Sony Music, ambayo itamsimamia kutoa album tano hiyo ikiwa ni pamoja katika suala zima la uandaaji na usambazaji.

Kampuni hiyo imedhamiria katika kuwawezesha wasanii wa hapa nchini na imekuwa ikifanya hivyo kwa wasanii mbalimbali duniani ikiwemo wale maarufu kama vile Usher, Chris Brown, Toya Delazy, Beyonce, Pitbull, Tumi and the Volume, J Cole and R Kelly.

Hakika unaweza kuwa mwaka wa bahati na Mungu ameendelea kumwinua mwanamuziki huyo.

Mwimbaji mwingine wa muziki wa injili nchini ambaye  nyimbo zake zimeendelea kukonga nyoyo za Watanzania ni Christina Shusho mbali na kuzindua albam ya nipe macho mwishoni mwa mwaka jana pia alibahatika kuingia kwenye kinyang'anyiro cha kuwania tuzo za ‘Africa gospel music awards  Julai 7 mwaka huu huko jijini Uingereza.

Pia Shusho kutokana na umahiri wake katika kuimba nyimbo za Injili umemuwezesha kutambulika vyema na kujinyakulia tuzo mbalimbali ikiwemo Tuzo aliyopata huko Nairobi, Kenya.

Shusho alikuwa kati ya wasanii wa nchini waliopata Tuzo za Muziki za Afrika Mashariki na Kati (EMAS) zilizofanyika Agosti 20, mwaka huu na kushirikisha wasanii mbalimbali wa kutoka nchi nane za Afrika Mashariki na Kati.

Mwimbaji huyo aliibuka na Tuzo ya Msanii Bora wa Kike wa Nyimbo za Injili akiingia na wimbo wake unikumbuke na kumshinda mwimbaji mwenzake kutoka nchini Upendo Nkone aliyeingia na wimbo wake Haleluya Usifiwe, Alice Kamande kutoka Kenya na wimbo wake Upendo na Gaby kutoka Rwanda na wimbo wake Amahoro.

Kati ya nyimbo ya Shusho ambayo imeendelea kufanya vizuri ni ile ya kuabudu iitwayo ‘nataka ushirika na wewe’ pamoja na wimbo unaosema ‘Nina wimbo’ ndizo zinazoongoza kuchezwa katika televisheni na redio mbalimbali nchini na nje ya nchi.

Pia mwimbaji wa mwingine wa injili kutoka nchini Kenya Solomon Mukubwa ambaye Aprili 8, 2012 alizindua albam yake inayokwenda kwa jina la ‘Kwa Utukufu wa Mungu’ yenye nyimbo nane na inayoendelea kufanya vizuri ni inayokwenda.

Nyimbo zilizomo katika albam hiyo ni pamoja na Kwa utukufu wa mungu wenyewe ambayo imebeba albam, Usikate tamaa, Mungu wangu Nitetee, Moyo wangu mtukuze bwana, Niko wa Yesu, Mke si nguo, Yesu jina zuri na Chunga ahadi yako.

Mwimbaji mwingine wa muziki wa injili ambaye ameweza kufanya vizuri ni Bahati Bukuku ambaye ameweza kutambulisha albam yake ya  Dunia Haina Huruma iliyobeba nyimbo nane ambazo ni Wewe ni Baba, Dunia Haina Huruma iliyobeba albam, Ahabu,Maamuzi, Atakushangaza, Abneli, Mbeba Maona na Kampeni

Aidha mwambaji Martha Mwaipaja anaweza kuwa ni mwimbaji aliyefanya vyema katika muziki wa injili baada ya kutamba kwa muda mrefu na albam yake ya ‘Usikate Tamaa’ na mwaka huu kuachia album yake mpya inayobebwa na wimbo wa Ombi langu kwa Mungu

Nyimbo zilizomo katika album hiyo ni ile inayobeba albam ya ‘Ombi langu kwa Mungu’ nyingine ni Jaribu kwa mtu, Adui wa mtu, Yesu ni mzuri, kweli nimetambua, kaa na mimi tena, nani ajuaye maumivu, pamoja na sifa zivume huku wimbo wa kaa na mimi tena akiwa amemshirikisha mtangazaji wa Wapo Radio Fm ambaye pia ni mwalimu wa kwaya ya New Jerusalem kutoka EAGT Mito ya baraka Silas Mbise.

Martha ambaye ameolewa machi 4 mwaka huu na mchungaji mchungaji John Said, ambapo inaelezwa kuwa ameweza kupata mafanikio mengi sana kiroho na kimwili kiasi kwamba hawezi kueleza yote.

Wapo waimbaji wengi wa nyimbo za injili walioweza kufanya vema mwaka huu lakini hawa ni baadhi ya wachache ambao kazi zao zinaendelea kuinua mioyo iliyoinama na ile ambayo inaitaji faraja ya Kiungu.

WANENGUAJI WA TWANGA JUKWAANI


Wanenguaji wa Bendi ya African Stars “Twanga Pepeta” wakioingozwa na kiongozi wa wanenguaji Asaha Said  wa kwanza kushoto , Mandela Sura Mbaya katikati  wakionesha umahiri wao wa kunengua jukwaani katika moja ya maonesho ya bendi hiyo hivi karibuni.

Monday, 17 December 2012

KOFFI KUTOA BURUDANI DAR ES SALAAM



MSANII Antoine Agbepa Mumba almaarufu kama Koffi  Olomide (56) ambaye  ni mahiri  katika uimbaji wa miondoko ya Soukous  yupo nchini kutoa burudani  Jumamosi  Desemba 15 2012.
Ni msanii mwenye majina mengi yaliyompa umaarufu kama Grand Mopao, Mokonzi, Tcha Tcho king, atatumbuiza  na bendi yake  ya Quartin Latin  katika uwanja wa Leaders Club Kinondoni jijini Dar es Salaam.
 Akiwa nchini kwa  uratibu wa Kampuni ya Prime Time Promotions Olomide ametua na muimbaji nyota wa bendi hiyo Sindy ambapo watapamba miaka 13 ya kuanzishwa kwa Kampuni ya Clouds FM.
Mbali ya bendi ya Koffi pia bendi pinzani nchini FM Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ wakiwa chini ya uongozi wa Kyala Matala ‘Nyoshi El Saadat’ watatoa burudani sanjari na bendi ya The African Stars Entertainment ‘Twanga Pepeta’ nao wamesema kwamba wamejipanga kwa kutoa burudani kesho.
Akizungumza jana Kiongozi wa Twanga Luiza Mbutu anasema kwamba watatumia onesho hilo kwa kujifunza muziki kutoka kwa Koffi kwani kundi hilo linaongozwa  nha nguli wa muziki duniani.

Aidha katika hali nyingine haijawahi kutokea kwa bendi mbili pinzani za Twanga na FM Academia kupanda katika jukwaa moja na onesho moja  hivyo  siku ya kesho itakuwa ni siku maalumu kwa wapenda muziki kupata burudani kutoka kwa bendi mbili kubwa nchini na moja ya kimataifa.
Bendi nyingine itakayosindikiza katika onesho hilo ni Skylight  iliyozinduliwa mwaka huu.Kiingilio ni sh.10,000 kabla na sh. 15,000 mlangoni.
Alikotoka
Koffi  Ambaye ni mwanamuziki mahiri msomi pia mtunzi mzuri wa nyimbo  amabye alianza kuonesha umahiri wake kati ya mika 1970 na 1980 ambako alikua akimuandikia nguli wa muziki nchini Janhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Papa Wemba enzi hizo akiwa na bendi ya  Orch Viva La Musica.

Wakongomani wengi wanamkubali  Koffi Olomide kuwa yeye ni chuo cha mafunzo kwa wanamuziki wengi wa DRC, mmoja wa wanao ukubali ujabali wa muziki wa Olomide ni pamoja na mwanamuziki wa kikongo anayeishi jijini Nairobi nchini Kenya Kasongo wa Kanema  anayetumikia katika bendi ya Super Mazembe hukuakisema “Koffi ni msafi katika muziki na tungo zake pia kwani ujumbe anaoutoa unakuwa wenye uzito na maana kubwa”.
“Nyimbo nyingi za Olomide ziko kipekee na ikipigwa tu utatambua kuwa sasa mopao yuko hewani,kutokana na ujuzi wa aina yake  mpangilio murua  ndio unaompatia mrehjesho mzuri, kuuza vema kazi zake na kumpatia umarufu”anasema Kanema.
Kasongo anasema kwamba kupendwa kwa muziki wa Koffie sio kwamba kumekuja bure amesoma , amejituma na huumiza kichwa kila anapotaka kuachia albamu hio ndiyo siri kubwa ya muziki wa Koffie.
Kwa wadau wa muziki watakumbuka moja ya kibao kilichotamba kuwa ni 'Papa Plus', 'Futa Djalon', 'Andraa', 'Loi', 'Mbirime', 'Micko', 'Attentat' na 'Ngounda'.
 Pia Koffi amewahi kurekodi na mwanamuziki Nyboma Mwanindo wimbo wa 'Anicet' na 'Papa Bonheur'
Changamoto  katika muziki
Kwa muda wa miaka mitatu iliyopita mwanamuziki huyu  hakuweza kufanya maonesho barani Ulaya kutokana nakukabiliwa na kesi ya kunyanyasa wacheza shoo wake huku wakihusishwa na masula ya kisiasa anti-Kabila.
Koffi aliwekwa chini ya ulinzi Agosti 15, jijini Kinshasa, pia alitetewa na jopo la mawakili wapatao 10.
Kama ilivyo kawaida ya wanamuziki siku zote kusaka maslahi yao ,mwaka 1998 Koffi alionja chungu  ya muziki baada ya onesho kubwa lililofanyika kwenye ukumbi wa Olympia  jijini Paris bendi yake ilivunjika.
Ilivunjwa na baadhi ya wanachama na wanamuziki walioenda kuanzisha  bendi ya Orchestre Quartier Latin Academia.
Historia yake kwa ufupi
Alizaliwa Julai13, 1956, Kisangani kabla familia yake haijahamia Kinshasa DRC huku mama yake akiwa mwenye asili ya huko na baba yake ni mwenye asili ya kutoka nchini Sierra Leone.
Ametoka katika familia yenye maisha na uwezo wa kati  
Mwaka 1970  akitokea nchini Ufaransa alijiunga na  bendi ya Viva la Musica  iliyokuwa ikimilikiwa na  Papa Wemba ambapo alikuwa katika nafasi za ‘ music composer’ na mwandishi wa nyimbo na baadaye akaja kuwa mwimbaji mahiri.
Mwaka 1986, alilipa kisogo kundi la Viva la Musica  na kuanzisha  bendi yake ya Quartier Latin,ambayo ilikuwa imesheni  ala zote za muziki, waimbaji,  na wacheza shoo huku kundi zima likiwa na wanamuziki wapatao 30.
Kuanzia hapo Koffi ndipo alipokunjua makucha yake na kujijengea jina Afrika Mashariki, Kati, Kusini na Afrika Magharibi akitamba na Tcha Tcho mtindo wa soukous.
Mwaka 2002 alipata tuzo ya muziki ya Kora Award  akiwa kama mwanamuziki bora Barani Afrika.
Mafanikio
Wanamuziki wengi wenye asili kutoka nchini  DRC wengi wamepita katika mikono yake  kama vile Fally Ipupa, ambaye Koffi alimpika kwa muda wa miaka 10  ndani ya bendi yake ya Quartier Latin , kabla mwanamuziki huyo hajaamua kua solo na hatimaye kuanzisha bendi yake.
Kwa sasa  Fally  ni kati ya  mwanamuziki wenye heshima na jina kubwa duniani ambaye anafanya kazi na kuisshi nchini Marekani huku akifanya kazi kwa karibu na G-Unit of 50 Cent’s Olivia.
Nyota mwingine katika muziki aliyepitia katikia mikono ya Koffi ni Ferre Gola, baada ya kuachana na kundi la Werra Son Wenge Musica Maison Mere.
Kama hiyo haitoshi  tunda lingine adhimu la kazi ya Koffi ni Montana Kamenga ambaye baada ya kujiona amewiva kimuzi kutoka kwa Koffi alikimbilia kwa General Defao Matumona.

Pia wengine waliopikwa na Koffi ni  Fele Mudogo, Sam Tshintu, Suzuki 4x4, Buro Mpela na Soleil Wanga.
Kutokana na umahiri wake katika muziki Koffi amewahi kushirikishwa katika  miradi mbalimbali ya muziki ikiwa ni pamoja na ‘Salsa music project’, ‘Africando music project’.
Albamu:
Effrakata, Tcha Tcho, Magie, Haute De Gamme- Koweit, Rive Gauche, Pas de Faux Pas, Live A Bercy, Attentant, Ngounda, Le Rambo du Zaire, Golden Star,  Noblesse Oblige, V12, Ultimutum, Loimore, Monde Arabic na Abracadabra inayotamba hivi sasa.
Makala imeandaliwa na Khadija Kalili na Msaada wa Mashirika. 


Wednesday, 12 December 2012

RAY C AMSHUKURU RAIS KIKWETE KWA MATIBABU


 
MSANII wa muziki wa kizazi kipya  (Bongo fleva) Rehema Chalamila ‘Ray C’, juzi ametinga Ikulu kufikisha shukurani zake kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na kumpatia msaada wa matibabu.
Ray C aliyefuatana na Mama yake Mzazi Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve, alimweleza Rais kuwa afya yake imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kwa ajili kukonga nyoyo za mashabiki wake waliyomkosa kwa muda sasa.
Kwa apande wake, mama mzazi wa Ray C, alisema anamemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye kwani hali ili kuwa ya kusikitisha wakati alipokuwa akiumwa.
Aidha mama Ray C amesikitishwa na baadhi ya watu kutumia fursa ya matatizo ya mwanaye kuwa chanzo cha kujipatia fedha kwa kukusanya michango eti  kwa ajili ya matibabu.
Mama Ray C aliongeza kwa kuwataka baadhi ya watu amnbao wanafanya vitendo hivyo kuacha mara moja kwa kuwa kwani matibabu ya Ray  C yamegharamiwa na Rais.