
MSANII wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) Rehema Chalamila ‘Ray C’, juzi
ametinga Ikulu kufikisha shukurani zake kwa Rais Jakaya Kikwete kutokana na
kumpatia msaada wa matibabu.
Ray C aliyefuatana na Mama yake Mzazi
Margareth Mtweve na Dada yake Sarah Mtweve, alimweleza Rais kuwa afya yake
imeimarika na kwamba muda si mrefu atarejea jukwaani kwa ajili kukonga nyoyo za
mashabiki wake waliyomkosa kwa muda sasa.
Kwa apande wake, mama mzazi wa Ray C,
alisema anamemshukuru Rais Kikwete kwa kuokoa maisha ya mwanaye kwani hali ili
kuwa ya kusikitisha wakati alipokuwa akiumwa.
Aidha mama Ray C amesikitishwa na
baadhi ya watu kutumia fursa ya matatizo ya mwanaye kuwa chanzo cha kujipatia
fedha kwa kukusanya michango eti kwa
ajili ya matibabu.
Mama Ray C aliongeza kwa kuwataka
baadhi ya watu amnbao wanafanya vitendo hivyo kuacha mara moja kwa kuwa kwani
matibabu ya Ray C yamegharamiwa na Rais.
No comments:
Post a Comment