
Muhando na Enock Jonas ‘Zunguka’ watapamba katika maalum la
kuchangia watoto yatima lenye lengo la kuielimisha jamii na kuamsha mwamko wa
kusaidia watoto yatima na wanaoishi katika maisha magumu.
Akizungumzia tamasha hilo Rose alisema amejiandaa
kusherekea Uhuru kwa aina yake tofauti na
watu wengi walivvozoea kwa kuwashirikisha watoto yatima na wale wanaoishi
katika mazingira magumu.
“Nimefurahi kupata nafasi ya kutumbuiza katika tamasha hili
la aina yake hasa katika mkoa wa Kagera
ambapo itakuwa mara ya kwanza kuonekana live katika mji wa Bukoba”, alisema .
Muhando aliwamba wananchi wa Bukoba kufika kwa wingi katika
tamasha hilo la kipekee katika ukuonyesha moyo wa upendo kushirikiana na
kusaidia jamii ya watu wengine wasio jiweza.
Alisema kupitia tamasha hilo anatarajiwa kuwapa uhondo wa
nyimbo zake za zamani sambamba na kutambulisha nyimbo zake mpya ambapo wakazi
wa huko watapata fursa ya kuzisikiliza kwa mara ya kwanza.
Naye Zunguka
amewataka wakazi wa Kagera kukaa mkao wa kula kwa ajili ya tamasha hilo na
watarajie kupata burudani ya kutosha na ya kipekee kutoka kwake ambayo itawajenga roho ya imani, kupendana na
kusaidia watu yatima na watoto wanaoishi katika mazingira magumu ili nao waweze
kufaraia maisha.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kampuni ya Beula
Communications Ltd, ambao ni waandaji wa tamasha hilo,Melkizedeck Mutta alisema
maandalizi yanakwenda vizuri na kuwataka wadau kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
Aliongeza kuwa mbali ya wasanii hao, pia tamasha hilo
litapambwa na burudani kutoka bendi ya
muziki ya wazawa mkoa huo, Kakau Band pamoja na vikundi vingine vya
wanakwaya wa makanisa mbalimbali na kikundi cha watoto yatima.
No comments:
Post a Comment