DONNIE Mc Clurkin ni Mwanamuziki Mashuhuri wa nyimbo za Injili
na Mchungaji wa Kanisa la Perfecting Faith church lililopo katika jimbo la
Detroit nchini Marekani.
Donnie alizaliwa na familia ya Donald na Mama Frances Mcclurkin
Januari 25, mwaka 1959 na kukulia katika
mji wa Louisville.
Akiwa na umri wa miaka nane, mdogo wake wa kiume mwenye umri wa miaka
miwili aligongwa na gari na kufa papo hapo huku Donnie akishuhudia.
Wakati Donne akiwa na majonzi mazito usiku huo huo ambao
walimzika mdogo wake, mjomba wake alimbaka Donne.
Baada ya kifo hicho familia yake iliingia kwenye mgogoro kubwa
ambao ulitokana na utumiaji wa dawa za kulevya.
Muimbaji huyo alipofikisha miaka 13, binamu yake mtoto wa mjomba
wake alimbaka tena Donnie pamoja na dada zake wawili kitendo amabacho
kilimuumiza sana na kumuachia kovu la aina yake.
Anasema kuwa muda wote alijiona mkosaji, mtu aliyekandamizwa na
hakuwa na ujasiri mbele za watu na mwenye wingi wa aibu.
Kwa kipindi hicho chote anaeleza kuwa alipata faraja toka kwa
shangazi yake ambaye alikuwa muimbaji wa nyimbo za Injili.
Shangazi yake huyo alimfanya Donnie ajiingize kanisani na kuanza
kupiga piano na kuimba kwaya kama sehemu ya kufuta machungu na kuondokana na
msongo wa mawazo aliokuwa nao.
Mama yake mzazi naye alikuwa muimbaji kanisani hivyo kanisani
kukawa ndio nyumbani kwake na kambi yake pindi nyumbani kukitokea matatizo.
Julai 14, 1969 akiwa na miaka takribani kumi ikiwa ni jumapili
akiwa kanisani huko Amityville Gospel Tabernacle mtumishi wa Mungu aliyekuwa
akihubiri aliwaambia watu kuwa Kristo alikufa kwa sababu anakupenda wazo hilo ndilo lilikuwa kwa Mcclurkin ndipo
akaamua kuyakabidhi maisha yake kwa Yesu.
Kwenye kitabu alichoandika kuhusu maisha yake anasema “ Kanisa
limekuwa ndio ulimwengu wangu mahali ambapo najisikia amani na najisikia kama
ndio Mahali Pangu halisi”anaeleza.
Mwaka 1971 wakati ana miaka 11, alikuwa akimpenda sana
mwanamuziki mashuhuri wa nyimbo za injili kipindi hicho aliyeitwa Anre Crouch.
Anaeleza kuwa siku aliposikia kuwa Crouch anakuja katika jimbo
lao alimuomba mama yake ruhusa waende kwenye tamasha na kumuahidi jumatatu yake
ataamka mapema na kwenda shule kama kawaida.
Anaendelea kusema kuwa mama yake alikubali na wakaenda Tamashani
na Donnie akaaa mbele kabisa sambamba na mamaye.
Baada ya Crouch kuingia ukumbini saa tano usiku kabla hajaanza
kuimba alimuona Donnie na kumfata, Donnie anasema, “Crouch akaniuliza kitu gani
unafanya hapa, nikamjibu nakusubiri wewe, akaniuliza kama nimelipenda tamasha nikamjibu
ndio, akanambia wakati yuko mdogo hakuweza kuimba wala kucheza mpaka baba yake
alipomuombea, Nikamjibu baba yangu hajaokoka hivyo hawezi kuniombea. Mwishoni
akaniuliza kama nitapenda aniombee nami nkamkubalia akaweka mkono wake kichwani
kwangu akasema “Mungu mpe kile ambacho umenipa mimi” kisha akaelekea stejini,
huuo ulikuwa ndio mwanzo wa hiki nlichonacho leo”anasema Donnie.
Akiwa kanisani hapo alianzisha kundi llilokuwa linajulikana kama
The Mcclurkin Singers na baadaye alianzisha kundi lililokuwa likijulikana kama
The New York Restoration Choir.
Mwaka 1983 wakati akiendelea kutumika na kwaya alikutana na
Pastor Marvin Winans.
Mchungaji Winans alivutiwa sana na namna Donnie alivyokuwa
akiimba kwenye semina ya injili.
Baadaye Winans alimwalika Mcclurkin katika mji wa Detroit
alikokua akiishi ili kumsaidia kuanzisha huduma kanisa liitwalo Perfecting
Faith Church.
Miaka sita baadaye Donnie aliamua kuhamia Detroit na kuanza
kufanya kazi na Pastor Winans.
Katika kipindi hicho anasema kuwa ndipo Mcclurkin alipata wasaa
wa kuzunguka sehemu mbalimbali na kufanya huduma akiwa chini ya pastor Winans.
Donnie anasema familia ya Winans imekuwa karibu sana na yeye
Kuanzia Bebe, Cece, na Pastor Marvin na wakati mwingine anafikiri yeye ni
Donnie Mcclurkin Winans.
Donnie Mcclurkin na Cece Winans wakiwa wameshikilia tuzo za
Trumpert awards walizopewa mwaka 2007
|
Akiwa na Pastor Winans, alisaini mkataba na kurekodi albamu yake
iliyoitwa LP, Albamu hiyo iliyokuwa na nyimbo kama Stand iliyongoza kwa
umaarufu na kuzinduliwa na Oprah Winfrey.
Nyimbo hiyo ilitunukiwa tuzo ya Grammy kwa mwaka huo wa 1996 kwa
upande wa nyimbo za Injili. Album zake tatu za solo zilikamata nafasi za juu
sana kwenye chati za Bilboard.
Akiwa na furaha ya ajabu Mcclurkin kupitia makongamano
mbalimbali huwasimulia watu ukweli wa maisha yake huku akipinga kwa nguvu
mahusiano ya jinsia moja.
Mcclurkin anaamini kwamba suala la Homosexuality ni suala la
kiroho haliwezi tibika kisaikolojia na linahitaji msaada wa Mungu pekee. Baada
ya watu wengi kuwa wanamuomba aelezee historia ya maisha yake, Mcclurkin
aliamua kurudi nyumbani kwao Amityville New York na kumuomba Mama yake ruhusa
ili aandike kitabu kuhusu maisha yake.
Frances Mcclurkin (mamaye), alimruhusu Donnie aandike kitabu
kinachoyaelezea maisha yake kinaga ubaga, ndipo Mcclurkin akatumia miezi 18
kuandika kitabu hicho ambacho alikiita Eternal Vitcting, External Victor.
Alisema aliamua kuandika kitabu sio kwa kusudi la kuweka wazi uovu uliokuwa
ukifanyika ndani ya Familia yao bali kwa sababu yeye ni Mwalimu, na mwalimu ni
vizuri ajitoe yeye kama ujumbe ili watu wengine wajue kuwa hawako peke yao
kwenye mambo wanayopitia.
Mwaka 2008 Mcclurkin alichaguliwa kuwa miongoni mwa wanamuziki
ambao watakuwa kwenye timu ya Barak Obama katika harakati za uchaguzi wa nchini
Marekani.
Mcclurkin alikubali na kujumuika na Barak Obama, lakini kutokana
na msimamo wake wa kupinga mahusiano ya jinsia moja, Mashoga wengi walipinga
kuwepo kwake kwenye timu ya Obama. Hivyo ili kupata kura za mashoga ilibidi
Mcclurkin atolewe kwenye orodha hiyo ingawa alifanikiwa kuimba kwenye moja ya
kampeni za Rais Obama
Makala hii imeandikwa kwa msaada wa mtandao na Happiness Mnale,
0712 00 35 39,barua pepe mnaleh@yahoo.com
mwisho
No comments:
Post a Comment