Rais wa (CHAMUITA) Addo November, katikati Mweka Hazina Upendo Kilahiro na Naibu Mwenezi John Shabani.
Na Khadija Kalili
MAPEMA wiki hii Rais wa Chama cha Muziki wa Injili
Tanzania (CHAMUITA) Ado November
ameitaka serikali kutokukimbilia mchakato wa kufanya usajili kwa kazi za
wasanii kwa kutumia stika moja bila ya kuweka mipango madhubuti ya kuwabana
wezi wa kazi hizo.
Akizungumza jana Dar es salaam November anasema
kwamba Serikali isikimbilie katika stika pekee bali watupie kwanza macho ya
kazi za wasanii zinazoibiwa sehemu mbalimbali kama kwenye mabasi, ambako
huoneshwa filamu na CD za miziki ya Injili huku msanii akiachwa bila ya kupata
faida yeyote.
“Sio hao ntu bali wezi wengine ni pamoja na waumini
wakuu wa dini ya Kikristo kwani nao
utawaona wakitoka katika nyumba za kuabudu Kanisani wanalipia fedha kidogo huku
wakidurufiwa CD huku wakichagua ,majina ya wasanii wanaotaka nyimbo na picha zao ,utasikia
wakitoa orodha ya majina ya nyimbo na albamu wanazozitaka, katika hili hata
mungu hatoweza kupokea sadaka zao wanazozitoa makanisani kwani wanafanya
dhuluma kwa watu wanaojinyima na kurekodi lakini wao badala ya kununua albamu
nzima wanaishia kuchoma CD” anasema November.
Anaongeza kwa kusema ,”Sisi kama CHAMUITA tumejipanga kuwekeza
katika elimu zaidi ili wasanii wa muziki wa Injili waweze kufahamu haki
zao kwanza kabla ya kuingia katika
mpango huo ambao ni mzuri kimaendeleo.
Wakati huohuo November anasema CHAMUITA
wamepiga hatua kubwa kwani hadi sasa
tayari wameshszindua ‘website’ ya chama
itakayofahamika kama www.gospal Tanzania.com ambapo wasanii ambao ni wanachama wataweza
kujitangaza kwa kuuza picha, nyimbo na zao
kwa kupitia mtandao huo
Wakati huohuo mjumbe wa CHAMUITA , Bahati Bukuku
amezungumza kwa niaba ya waimbaji wengine wa muziki wa Injili kwamba serikali
sikurupuke katika suala la uanzishwaji wa kutumia stika moja kwani itawabebesha
mzigo wasanii na kazi zitaendelea kuibiwa zaidi.
“Wizi wa kazi za sanaa ni janga la Taifa hivyo kila
Mtanzania anapaswa alipigie kelele, hiki ni kilio cha umma sisi wasanii
hatukubaliani kwamba kila msanii atatumia stika moja , hapo wizi utaendelea
kwanini wasitumie mfano wa kadi za benki huku kila mmoja akawa na namba au neno
lake la siri ili kila msanii ajue
anakwatwa kodi kwa namna gani na kwa
kutokana na kopi ngapi kulingana na
kipato chake lakini ikiwa stika moja wapo wasanii watakaopandia kwa kupitia
jina la mwingine”anasema Bukuku.
MALENGO NA MADHUMUNI
November anasema CHAMUITA Itaendeshwa kama
chombo kisicho na malengo ya kupata faida na kitakuwa na malengo na madhumuni
yafuatayo anayoyataja, Kulinda utamaduni wa Tanzania na heshima ya muziki wa Injili,
Kuhamasisha maendeleo ya muziki wa Ijili na nyaja zake nyingine,Kutoa ushauri
katika mambo yote yahusuyo muziki wa Injili.Kuwakilisha na kulinda maslahi ya
wanachama kitaifa na kimataifa, Kuwa chombo cha kuwezesha mawasiliano kati ya
watu na vikundi katika kupeana taarifa kuhusu muziki wa Injili, Kuwa na rejista
ya wanamuziki wa Injili na kazi zao. Ili
kusaidia kulinda na kutangaza haki za wanachama, Kutafuta mapato kwa njia ya
ada, michango, harambee, maonyesho, kukopa, ufadhili au zawadi katika
kuendeleza malengo na madhumuni ya Chama, Kuwezesha mawasiliano ya kitaifa na
kimataifa, Kuwawezesha wanamuziki wa Injili kwa njia ya kuwaongezea elimu, Kuinua
hadhi ya muziki wa Injili nchini,Kutambuliwa rasmi na Serikali yetu na wadau
wengine Tayari tumesajiliwa na BASATA na kupewa usajili rasmi na Kuwekeza katika miradi, na kujipatia kipato
kwa nia ya kuwakomboa jamii ya wanamuziki wa injili.
Changamoto
kwa wasanii
Wasanii
mbalimbali ambao walihudhuria mkutano uliratibiwa na Mamlaka ya Mapato nchini
(TRA), walilazimika kutofikia muafaka katika mkutano huo na baadhi ya viongozi
waliofika kuzungumzia mpango wa uwekwaji wa stika ifikapo mwakani.
Chama chetu kinaundwa na Mwanamuziki mmoja mmoja
yaani solo artist, vikundi, umoja wa Makundi yote ya Muziki wainjili hapaTanzania, kwa kuhusisha radio,
watangazaji, wapigaji na wadau wa muziki wa injili.
Safu ya uongozi (CHAMUITA ) Addo November ,Makamu
Mchungaji Joseph Malumbu , Katibu David
Robert , Katibu Mwenezi Stella Joel, Naibu Mwenezi John Shabani, Mweka Hazina Upendo Kilahiro.
Wajumbe wa Kamti Kuu wako zaidi
ya 60 huku baadhi ni wakiongozwa
na Mbunge Matha Mlata, Mzee Makassy, Cosmus Chidumule, Bahatgi Bukuku, Ency
Mwalukasa, Christine Shusho, Levina Steven, Mzee Mutash, Jojo Josee , Jackson Bent,
Fred Rwesasira.
Mikakati
ya Chama
November anasema kuwa tayari wameshazungumza na
wanachama wao ikiwa ni pamoja na kuweka mikakati ambayo wamejiwekea ambayo ni kuunganisha
wanamuziki wote wa injili na wadau wao na kuwapa nguvu katika majukumu yao ya
kila siku, pamoja na kutetea haki za msingi za wanamuziki.
Kuwakumbusha wanamuziki juu ya umuhimu wa CHAMA na
kuishi maisha ya kumpendeza Mungu, Kutetea haki za wanamuziki na kutoa wito kwa
jamiii na serikali kwa ujumla wa kutambua wizi
wa kazi za sanaa kama janga la kitaifa kwani wanamuziki wanakosa mapato na
serikali inakosa kodi ambayo inaweza kuzidi hata mapato ya maliasili na utalii
au madini, mfano kazi moja tu ya mwanamuziki mmoja akauza nakala milioni 4 kati
ya watanzania milioni 40 waliopo mwanamuziki huyo anaweza kupata bilioni 4 kwa kanda
ya shilingi 1000 tu.
November
anasema tunaungana na kauli hii ya Shirikisho la Muziki Tanzania kuwa
umefika wakati sasa wanamuziki tuseme basi katika kuibiwa kazi zetu za sanaa , tunawataka viongozi
wan chi wakae pamoja nasi tuwape mikakati yetu wasikae mbali
na sisi kwani tuna uwezo wa
kukuza uchumi.
Kutoa mafunzo kwa wanamuziki kuhusiana na muziki na
haki miliki, pamoja na kuwekeza katika maisha
ya baadaye tayari kuna wadau
kutoka LAPF tayari wametoa mada na
kuandikisha wanachama, hii ni fursa kwao kujipatia mikopo ya nyumba na kuwekeza
katika akiba yao ya baadae.
Kutoa mapendekezo juu ya mabadiliko ya sheria yetu
ya haki miliki ambayo kiukweli haina meno na imepitwa na wakati. Leo tunatoa
dukuduku chetu juu ya Sheria inayolinda kazi za wanamuziki na wasanii wengine
(The Copy Rights and Neighbouring Act no 7 of 1999) mfano suala la faini
isiyozidi milioni tano, kwani sheria haisemi kazi hizo feki zinapelekwa wapi na
faini hii imekuwa ndogo mno na pia inatoa mwanya kwa watafsiri sheria ambao
mara nyingi tumejionea wakitoa hukumu ya mwizi kulipa faini ya laki mbili au
elfu sabini na kurudishiwa kazi yake ya wizi maana sheria ipo kimya.
Tunatoa pongezi wa Rais Kikwete kwa kukubali
mchango wa Chama mcha muziki wa injili na kukubali kuwa chama pekee
kilichoshiriki kuimba katika miaka 50 ya uhuru pale uwanja wa taifa.
Hata hivyo tunatoa rai kwa viongozi wa serikali
kushirikisha makundi mbali mbali ya sanaa katika mchakato mzima wa kutetea haki
za wanasanaa wote kwani hiii itawapa fursa kufanya mambo yatakayokidhi haja za
wanamuziki na sanaa kwa ujumla.
Tunawashukuru wanamuziki wa injili na wdau mbali
mbali kwa jinsi walivyojitoa katika kumzika mzee wetu, Remmy Ongala, waandishi
waliopata ajali wa radio za injili ambapo chama kilijitoa kuwaona na
kuwafariji, msiba wa Fanuel Sedekia na
kusaidia waathirika wa Gongo la Mboto kazi hii ilifanyika kwa ufanisi mkubwa na
mzee wetu Remmy alizikwa kwa heshima kubwa, tunawaomba tuzidi kushikamana.
“Tunashukuru
sasa tumezindua uzinduzi website ya kwanza kutoka kwa wanamuziki wa
Tanzania, ambayo ni www.tanzaniagospel.com iliyotengenezwa
na Kampuni ya Spice Olyympus.
pamoja na
haya bado tunajipanga kuwatafutia wanamuziki wa injili mafunzo zaidi ya
kuwafanya kujitegemea na kusaidia maendeleo ya nchi” anasema November
Mwisho November anamalizia kwa kutoa pongezi za
dhati na shukrtani kwa LAPF kwa kudhamini mkutano wao na kuwaomba wanachama kuwaunga mkono katika
jitihada zao za kuwa komboa watanzania.
No comments:
Post a Comment