Na Betty Kangonga
UNAPOZUNGUMZIA albamu ya nyimbo za muziki wa injili
zilizofanya vema kwa mwaka 2012 ni pamoja na iliyoibwa na mwimbaji wa nyimbo za
injili ambaye anakuja juu anayefahamika kuwa ni Enock Jonas.
Moja ya nyimbo inayofanya vizuri na ambayo
imekuwa ikipigwa katika sherehe mbalimbali na hata hafla ni ile inayokwenda kwa
jina la wema wa Mungu ‘Zunguka Zunguka’.
Jonas ambaye katika albamu hiyo amefanikiwa
kutunga nyimbo zingine nane ambazo ni ufanikiwe, ukimtegemea Mungu, Haleluya
nakuabudu Bwana, ndugu zangu, ni vyema na ile
inayosema leo ni furaha.
Mwimbaji mwingine ambaye albam yake inaendelea
kufanya vema ni malkia wa nyimbo za injili nchini Rose Mhando ambaye
aliitambulisha album yake ya nne inayokwenda kwa jina la Utamu wa Yesu.
Albam hiyo ambayo inafanya vema katika vituo
mbalimbali vya redio na televisheni za ndani na nje ya nchi.
Mhando katika nyimbo yake ya Utamu wa Yesu na
raha ya ajabu anasema “Nimeonja utamu wa Yesu, Ukitaka gari nzuri, majumba
mazuri onja utamu wa Yesu”.
Kama usemi mmoja unavyosema kuwa aliyenacho
anaongezewa ndivyo ilivyokuwa kwa mwaka huu kwa upande wa malkia huyo kwani
aliweza kuingia mkataba mnono na kampuni ya Sonymeingia mkataba mnono na
kampuni mahiri katika masuala ya muziki na burudani hapa ulimwenguni,Sony
Music.
Rose Muhando ambaye anakuwa msanii wa kwanza wa
muziki wa injili nchini Tanzania kuingia mkataba wa kampuni ya Sony Music,
ambayo itamsimamia kutoa album tano hiyo ikiwa ni pamoja katika suala zima la
uandaaji na usambazaji.
Kampuni hiyo imedhamiria katika kuwawezesha
wasanii wa hapa nchini na imekuwa ikifanya hivyo kwa wasanii mbalimbali duniani
ikiwemo wale maarufu kama vile Usher, Chris Brown, Toya Delazy, Beyonce,
Pitbull, Tumi and the Volume, J Cole and R Kelly.
Hakika unaweza kuwa mwaka wa bahati na Mungu
ameendelea kumwinua mwanamuziki huyo.
Mwimbaji mwingine wa muziki wa injili nchini
ambaye nyimbo zake zimeendelea kukonga
nyoyo za Watanzania ni Christina Shusho mbali na kuzindua albam ya nipe macho
mwishoni mwa mwaka jana pia alibahatika kuingia kwenye kinyang'anyiro cha
kuwania tuzo za ‘Africa gospel music awards
Julai 7 mwaka huu huko jijini Uingereza.
Pia Shusho kutokana na umahiri wake katika
kuimba nyimbo za Injili umemuwezesha kutambulika vyema na kujinyakulia tuzo
mbalimbali ikiwemo Tuzo aliyopata huko Nairobi, Kenya.
Shusho alikuwa kati ya wasanii wa nchini
waliopata Tuzo za Muziki za Afrika Mashariki na Kati (EMAS) zilizofanyika
Agosti 20, mwaka huu na kushirikisha wasanii mbalimbali wa kutoka nchi nane za
Afrika Mashariki na Kati.
Mwimbaji huyo aliibuka na Tuzo ya Msanii Bora wa
Kike wa Nyimbo za Injili akiingia na wimbo wake unikumbuke na kumshinda
mwimbaji mwenzake kutoka nchini Upendo Nkone aliyeingia na wimbo wake Haleluya
Usifiwe, Alice Kamande kutoka Kenya na wimbo wake Upendo na Gaby kutoka Rwanda
na wimbo wake Amahoro.
Kati ya nyimbo ya Shusho ambayo imeendelea
kufanya vizuri ni ile ya kuabudu iitwayo ‘nataka ushirika na wewe’ pamoja na
wimbo unaosema ‘Nina wimbo’ ndizo zinazoongoza kuchezwa katika televisheni na
redio mbalimbali nchini na nje ya nchi.
Pia mwimbaji wa mwingine wa injili kutoka nchini
Kenya Solomon Mukubwa ambaye Aprili 8, 2012 alizindua albam yake inayokwenda kwa
jina la ‘Kwa Utukufu wa Mungu’ yenye nyimbo nane na inayoendelea kufanya vizuri
ni inayokwenda.
Nyimbo zilizomo katika albam hiyo ni pamoja na Kwa
utukufu wa mungu wenyewe ambayo imebeba albam, Usikate tamaa, Mungu wangu
Nitetee, Moyo wangu mtukuze bwana, Niko wa Yesu, Mke si nguo, Yesu jina zuri na
Chunga ahadi yako.
Mwimbaji mwingine wa muziki wa injili ambaye
ameweza kufanya vizuri ni Bahati Bukuku ambaye ameweza kutambulisha albam yake
ya Dunia Haina Huruma iliyobeba nyimbo
nane ambazo ni Wewe ni Baba, Dunia Haina Huruma iliyobeba albam, Ahabu,Maamuzi,
Atakushangaza, Abneli, Mbeba Maona na Kampeni
Aidha mwambaji Martha Mwaipaja anaweza kuwa ni
mwimbaji aliyefanya vyema katika muziki wa injili baada ya kutamba kwa muda
mrefu na albam yake ya ‘Usikate Tamaa’ na mwaka huu kuachia album yake mpya
inayobebwa na wimbo wa Ombi langu kwa Mungu
Nyimbo zilizomo katika album hiyo ni ile
inayobeba albam ya ‘Ombi langu kwa Mungu’ nyingine ni Jaribu kwa mtu, Adui wa
mtu, Yesu ni mzuri, kweli nimetambua, kaa na mimi tena, nani ajuaye maumivu,
pamoja na sifa zivume huku wimbo wa kaa na mimi tena akiwa amemshirikisha
mtangazaji wa Wapo Radio Fm ambaye pia ni mwalimu wa kwaya ya New Jerusalem kutoka
EAGT Mito ya baraka Silas Mbise.
Martha ambaye ameolewa machi 4 mwaka huu na
mchungaji mchungaji John Said, ambapo inaelezwa kuwa ameweza kupata mafanikio
mengi sana kiroho na kimwili kiasi kwamba hawezi kueleza yote.
Wapo waimbaji wengi wa nyimbo za injili
walioweza kufanya vema mwaka huu lakini hawa ni baadhi ya wachache ambao kazi
zao zinaendelea kuinua mioyo iliyoinama na ile ambayo inaitaji faraja ya
Kiungu.
No comments:
Post a Comment